Longino alianza kupapasa mikono yake taratibu juu ya matiti yale na kuna muda àlikuwa àkiyaminya kwa upole na kumfanya Mercy ashtuke kama miguu ya kuku anayemalizikia kukata roho baada ya kuchinjwa.
Utamu ulimzidi Mercy hadi alijikuta hana blazia bali kalala kwenye kitanda cha Longino huku midomo ya kijana yule ikiwa imebugia titi la kulia na titi la kushoto likiwa linapewa kashikashi na mkono mwingine uliobakia.
Pumzi za Mercy zikawa zinapishana kwa kasi ya àjabu lakini Longino hakutaka kuacha kufanya yake hadi pale aliporidhika na kifua na kuanza taratibu kubusu tumbo alilobeba binti yule. Tumbo lililochukua kitovu kilichozama kwa ndani pamoja ngozi mororo ambayo kwa Longino wakati anaipapasa, alihisi kama anapapasa tumbo la nyoka au mjusi.
Mabusu hayo yaliendelea kumwagika kutoka katika kinywa cha Longino.na sasa yakawa yanaenda sambamba na mikono ya Longino kuingia ndani ya sketi ya Mercy. Sketi ambayo haikuwa imembana kama kimini bali ilikuwa imejiachia kama sketi za shule ya msingi. Hali hiyo ya sketi, ilimpa urahisi Longino kuyatabaruku mapaja ya Mercy kwa kuyapapasa na kuyashika shika kwa utaratibu kama achaguaye nyanya au embe.
Mikono mikakamavu ya Longino iliendelea kutalii kwenye mapaja ya moto ya Mercy na wakati huo Mercy alikuwa hajiwezi kutokana na yale mabusu aliyokuwa anapigwa sehemu mbalimbali.
Mercy akawa macho legevu na pumzi zikizidi kupishana bila kutoa nafasi ya kusubiri pumzi nyingine kutoka. Ungemuona, ungehisi labda anakata roho au ana kifafa.
Bado mkakati kabambe wa mikono ya Longino uliendelea kujipa raha taratibu kwenye mapaja ya Mercy huku sura zao wote wawili zîkionesha zipo katika hisia za mbali mno katika dunia hii.
Longino aliendeleza safari aliyoianza na safari hiyo ambayo ilitawaliwa na mikono, ilitaka kwenda hadi kushika lastiki ya chupi ya mwanadada yule kwa lengo la kuivua lakini hali hiyo ilipingwa vikali na Mercy.
Hakupinga kwa kuwa alikuwa hajatoa jibu kuwa kakubali, bali alipinga kwa sababu ilikuwa ni zaidi ya mapema kuvuliwa chupi na mwanakaka yule ambaye alibahatika sana kumchezea mwanadada yule kirahisi kuliko hata ilivyotegemewa.
"Hapana Long. Hatuwezi kufanya leo kwani bado mapema sana kukimbilia haya mambo. Hunijui sikujui, kwa nini kwanza tusijuane hasa katika afya na tabia?."Mercy alitoa ushauri baada ya Longino kukasirika kunyimwa mchezo.
"Mercy. Usione kama nimekutaka mapema sana kufanya mapenzi na wewe. Lakini nipo katika hamu mwenzako, na sifanyi kwa ajili ya kujiridhisha nafsi yangu bali kwa sababu nakuhitaji. Nakuhitaji sasa, na nitakuhitaji daima.Nitakuoa wewe Mercy na si mwingine."Mwanaume alijitetea kwa hisia kali. Lakini kwa bàhati mbaya Mercy alikuwa bado hajamwamini. Juzi tu, alikuwa anamtaka rafiki yake, leo hii anasema ànampenda na ànamuhitaji. Hiyo haikumuingia akilini Mercy na àlimwona Longino kama mchezeaji tu.
"Long nakupenda sana tena sana. Naomba ufahamu hilo. Nitakupa chochote utakacho katika mwili kwa sasa kasoro ngono tu! Magonjwa na mimba Long. Unanijua? Unazijua tabia zangu? Hamu ya kufanya ngono isikupeleke kaburini. Tuchukue muda wetu kwa àjili ya kujuana kwanza.
Usidhani labda mi sina hamu. Nina hamu na wewe hata tufanye hadi asubuhi, lakini haiwezekani Long. Nahitaji kukujua japo kiafya,tabia tutarekebishana tu. Naomba unielewe."Longino alikuwa kimya wakati dada yule akionesha kuwa hakufika kidato cha tano bure, elimu yake anaweza kuitumia ipasavyo hata kwenye ushauri.
"Sawa Mercy. Nimekuelewa na samahani kwa nilichotaka kufanya. Nisamehe mpenzi wangu."Longino alimwomba msamaha dada yule na bila hiyana Mercy alielewa maneno hayo ya msamaha.
Walikuwa kama tayari wameshafanya kile kitendo, kwani baada ya kupeana misamaha, kila mmoja àlijirekebisha kimavazi na kuanza kuongea mambo mengine ambayo yalijenga zaidi mahusiano waliyoyaanzisha siku ile.
"Saa nane natakiwa kurudi kambini. Tutaonana baada ya wiki mbili kwa kuwa tutaenda kucheza na mechi huko Tunduma." Longino alimwambia maneno hayo Mercy na kuifanya hali ya furaha ya kimwana yule ipotee ghafla kama vumbi linapokutana na maji.
"Ndio nakwambia hivyo totoo."Longino alijibu huku akishika nywele ndefu za mwadada yule.
"Basi mi nataka."Mercy maneno yalimtoka kwa kudeka huku akimsogelea Longino ili amchezee na mwisho wangonoke.
"Wataka nini sasa?."Longino aliuliza huku akitabasamu kwa kituko anachotaka kukifanya Mercy.
"Nataka hiyo."Swali likajibiwa na Mercy huku akioneshea sehemu ya zipu katika suruali ya Longino. "Hapana totoo. Ujue mimi niliingiwa na shetani la tamaa za mwili tu. Ila kama ningefanya na wewe, leo mazoezini ningekoma. Leo Jumatatu tunapigaga mazoezi magumu sana kufidia siku zote tulizokaa nyumbani. Na pia, tujenge uaminifu kwanza ndio tuingie huko. Michepuko mingi sana kwa sasa, si rahisi mimi kukuamini wewe wala wewe kuniamini mimi.Tuaminiane kwanza. Mwili wako upo, na wangu ùpo. Kama ukifa àu nikifa,hayo ni ya MUNGU, ila kwa sasa, ningependa tufahamiane afya zetu, kama ulivyotaka."Longino aliongea hadi akamfanya Mercy atabasamu kwa kuona sasa kapata mtu muelewa.
"Nakupenda Longino. Sina cha kukwambia zaidi ya hicho." Mercy alimkumbatia Longino huku akitamka maneno hayo.
"Nakupenda pia Mercy. Utakuwa kama Mussa kwa wana wa Islael. Umekuja kuukomboa moyo wangu toka katika fukwe za mateso ya mapenzi. Nitakupenda daima."Sauti yenye maneno matamu ilipenya vyema kwenye masikio ya Mercy na kumfanya Mercy ahisi kama yupo peponi karibu na Malaika. ***** Siku hiyo nzuri kwa wapenzi wale ikaishia kwa kwenda kumchukua Jesca shuleni alipokuwa anasoma na kurudi naye kwa furaha huku Mercy akiwa mstari wa mbele kumpenda mtoto yule kwani alifahamu umuhimu wa kuuteka moyo wa Longino kwa kupitia pendo atakalompa mdogo wake.
Baada ya kukaa wote kwa muda, hatimaye ulifika ule muda wa Longino wa kurudi kambini. Muda ambao ndio kapangiwa na kocha wa timu ile ya chunya. Bila hiyana alimuaga mdogo wake ambaye alikuwa katika majonzi kiasi kwa kuachwa na kaka yake kipenzi, lakini hakuwa na jinsi kwani kaka alienda kutimiza ndoto zake.
Kwa upande wa Mercy, yeye alimsindikiza hadi kituo kidogo cha kupandia magari yaendayo Wilayani. Walipofika huko, walibusiana kidogo na Longino alipanda gari huku akimwachia maneno machache ya “Nakupenda sana Mercy”, naye Mercy alijibu kwa aibu kuwa anampenda pia na hapo Longino alifunga kioo cha gari ile ndogo huku nje akimuacha Mercy akiondoka kurudi yalipo makazi yao. ******* Longino alipokuwa katika gari ile ambayo ilishaanza safari ya kumpeleka ilipokuwa kambi yao, alianza kumfikiria Mercy uzuri wake. Akayakumbuka yale mapaja yake laini kama manyoya ya sufi, akaenda mbali zaidi akakumbuka jinsi alivyobaniwa kumvua nguo ya ndani binti yule. Hapo akatabasamu kidogo na kujiona kuwa alitaka kufanya jambo la kipumbavu sana.
Mawazo hayakuishia hapo, mara ya kuruka na kuanza kumuwaza Subira. Subira yule yule aliyemtupia vito vya shaba usoni. Subira mwenye mapozi kama anahela za kununulia hata kuku, kumbe hana chochote zaidi ya kumsubiri baba yake ajikune tako ili atoe wallet na yeye ndio apewe shilingi kadhaa za kwenda kununulia makochokocho ya kujipambia uso na mwili wake.
Eti ndiye aliyemtupia Longino vito usoni huku akivinadi kwa kebehi kuwa ni mabati. Hata kama ni mabati kweli, lakini ni zawadi. Tena zawadi ilitolewa fedha ili kununuliwa, sasa kwa nini aweke dharau zake kwenye kitu ambacho kimetolewa fedha? Au anajua labda Longino aliokota au alimuomba dada fulani mwenye navyo ndio akaletewa yeye. Wote hatujui, na itabaki kuwa siri yake. Siri iliyojazwa maswali kati yako msomaji na Longino muhusika.
“Nitamuonesha. Nitamuonesha kuwa dharau kwa mwanaume ni sumu kali ambayo hakupaswa kuionesha bali kukaa nayo moyoni.” Longino alijiwazia huku akigeukia upande wa kioo na kuanza kuangalia mandhari ya Jiji la Mbeya lakini mawazo hayakuwa katika mandhari hayo bali Subira. “Sijui nitalipa lini hiki alichonifanyia, ila nitalipa tu! Nitamuonesha kuwa uzuri wa simu siyo muonekano wake bali programu zilizowekwa ndani yake. Anajidai mzuri sana, sasa kikomo cha hayo yote kimekwisha. Pozi zote zitamshuka tu! Hatujui wanaume, hajui kuwa hata farasi akichoka goti huangukia, na hata maji ya yakizidi ubaridi sana hayaitwi tena maji, bali barafu. Nitamuonesha hayo yote, ila Mercy nitampenda daima japo huyu mbwa bado yupo moyoni kwa sasa.” Longino na mawazo yake ya kisununu yaliendelea kumtawala hadi akajikuta akipitiwa na usingizi. ****** BAADA YA WIKI MOJA.
Nyumbani anapoishi Longino kulikuwa kunafaraja mpya kwa familia ile. Mercy alikuwa kila mara hakosi kwenda nyumba ile na kuwasabahi mama mkwe pamoja na wifi yake Jesca. Kwa muda mchache tu! Mercy alikuwa kipenzi kikubwa cha familia ile. Ilifikia kipindi alikuwa hawezi kulala bila kwenda kuiona familia ya akina Longino. Ukweli ni kwamba , pale penye upele palipata mkunaji hasa. Na Mercy ndiye alikuwa mkunaji, alikuna kipele hata kile kidogo na kukisababishia kiwe kikubwa. Hapa nina maana kwamba, kipele kidogo ni imani ya Mama wa Longino ambayo ilikuwa moyoni mwake juu ya Mercy.Mama Longino hakuamini kama kuna mapenzi ya kweli katika mahusiano ya sasa. Alijua mwanaye anaenda kuumizwa na yule mwanamke hasa ukizingatia Longino aliishia kidato cha nne na Mercy alikuwa anaelekea kidato cha sita.
Mercy aligundua hilo, kile kipele kidogo akakikuna vizuri na kuwa kikubwa. Yaani ile imani ndogo ya mama yule, akaitanua na kuwa kubwa. Akaonesha kuwa anajali, akawa mstari wa mbele kuisaidia familia ile kwa kazi ndogo ndogo, na kilichompa pointi zaidi, ni kumjali Jesca. Jicho ambalo familia ile ilikuwa kama mbogo pale itakapoliona lina tatizo. Mercy akawa karibu kabisa na Jesca, naye Jesca akafurahia uwepo wa Mercy. Hapo moyo wa Mama Longino ukatua mzigo wa kumfikiria vibaya mtoto yule wa kike.
Mercy akapewa kibali ambacho hakikuwa cha moja kwa moja, lakini ni kibali ambacho alipewa kwa kuwa alionesha kujali. Ni hatua ndogo sana aliyoipiga lakini ilikuwa ni hatua kubwa kuliko zote katika maisha yake. Hatua kama ile ni wanawake wengi wanashindwa kuipiga kutokana na kujiwaza wao zaidi kuliko yule aliyefanikisha kumleta mtu yule wampendaye. Wanawake wengi wanadhani kumpata mwanaume ndio kumaliza kila kitu, hata wakikohoa dume litakurupuka lilipo na kuuliza kwa nini umekohoa.
Lakini wanasahau kuwa yule mwanaume ana familia. Yapaswa kuijali familia hiyo ili mwanaume aseme wewe ndiye unanifaa. Kama usipoijali familia ya mpenzi wako, sidhani kama utamjali na mwanaume kwani wewe utakuwa unamsumbua tu kuhusu familia yako. Mara mama anaumwa, mara baba anataka msuri, mara dada kafanyiwa oparesheni, na mengine kama hayo ambayo inafikia kipindi mwanaume anachoka na kuanza kujutia uamuzi wa kukuchukua. Hatua hiyo Mercy alijaribu kuipiga kabla hata hajaingia ndani zaidi ya familia ile. Heshima na utii alionesha kwa familia ile,sidhani kama kuna mwanamke wa kileo angefanya vile. **** Kwa upande wa Subira, yeye aliringa kwa kuwa wazazi wake walikuwa wana kitu cha kumpa. Si wazazi pekee, hata kaka yake aliyekuwa analangua vitu kutoka Dar es Salaam, alikuwa anamlinda dada yake na kumfanya aonekane ni dada wa kileo.
Vito vya thamani alivivaa Subira na ndio maana aliona kama utani pale alipoletewa shaba na Longino. Dharau zikamjaa mwanamke yule na kujiona kamaliza kila kitu. Licha ya kusoma kwake ambapo kungemfikisha mbali katika maisha yake, lakini ilimpasa kutambua pozi zikizidi mwili huwa ni kero kwa wengine. Kulikuwa hakuna haja ya kuwaletea pozi wanaume wanaokutaka hata kama ulikuwa unauwezo wa kuhamisha dunia kutoka sehemu kwenda nyingine. Kichwa kilimuuma Longino kwa matendo aliyotendewa na Subira, aliumia sana kwa matendo yale. Lakini kumbe hakuwa peke yake aliyefanyiwa yale. Vijana karibu wote walioenda kujaribu kumtaka, waliambilia shombo lililonuka kutoka katika kinywa cha msichana yule.
Sasa ni kijana gani wa kiume ambaye hakumpania Subira pale mtaani?. Na siyo vijana wa kiume tu! Hata baadhi ya wanawake wenzake walikuwa wanakereka na tabia zake, na kila mmoja alikuwa anamuombea siku moja adondoke. Lakini maombi yao yalikuwa kama dua la kuku tu, kamwe usitegemee litamtapata mwewe. Subira alizidi kugaa gaa kwa tambo pale mtaani kwao anapoishi.
Na alikuwa anahaki ya kugaa gaa na tambo hizo, kwani alikuwa mlimbwende wa sura hata umbile. Licha ya kutumia vipodozi mbalimbali, bado aliiheshimu sana rangi aliyojaaliwa na MAULANA. Rangi yake nyeusi kama uwajuavyo watu wa Mbeya, ndiyo ilikuwa inamfanya ang’are zaidi pale anapojipiga “make up”. Miguu na ngozi yake mororo kama niru ile inayotumiwa kutengeneza sakafu yenye mchanganyiko wa maji na saruji, ndivyo vilisababisha mtaa mzima usimame kwa muda wakati mrimbwende huyu anakatiza mbele yao.
Nani ambaye alikuwa hamjui Suby wa Minato na Pozi? Kifupi hakuna ambaye alikuwa hamjui. Na kwenye vijiwe vya karata na drafti, vijana wengi walikuwa wanatengeneza gazeti la kurasa nyingi tu zinazomzungumzia huyu Suby wa Minato. Pale walipopata taarifa kuwa mtu fulani kaenda kutoa hisia zake kwa mwanadada yule, walimsubiri kwa hamu atoke huko alipoenda ili aje kuwachekesha kwa alichofanyiwa. Matokeo yake Suby akawa mtu wa kujaribiwa na kila mwanaume. Kikundi kizima cha wacheza drafti na karata, kilipanga kwenda kumtongoza ili kuthibitisha kama kweli Subira alikuwa ana shombo. Walichokutana nacho, ilikuwa ni sawa na alichokutana nacho Longino.
Vijana wale ambao walionekana kama wahuni kutokana na kumalizia muda wao mwingi kwenye drafti, karata na ma-pool table, ambapo michezo hiyo ilitawaliwa na hela sana wakati wanaicheza, yaani ni kamali. Walipanga jinsi ya kumkomoa dada yule, dada mrembo mwenye pozi na njozi za kimalkia, mwenye nguvu ya mdomo wa shombo, mdomo wenye kiburi na wingi wa kejeri. Jinsi gani watamkomoa? Ni wao wenyewe wanajua. Ila mpango madhubuti ulipangwa kwa ajili hiyo. ****** Baada ya wiki zile mbili ambazo Longino aliahidi kuwa atakaa kambini, Longino alirudi huku akiwa anafuraha tele moyoni mwake. Furaha ya kumuona mdogo na mzazi wake pamoja na mpenzi wake mpya. Hiyo ilikuwa ni furaha iliyoambatana na shauku, shauku ambayo ilimkumba baada ya kufikiria ni vipi Mercy atapokea matokea aliyoyapata huko alipotoka.
Kulikuwa kuna matokeo mawili mazuri aliyapata huko alipokuwa amejichimbia yeye na timu yake. Kwanza ni matokeo ya mechi waliyocheza na timu ya Tunduma, ambapo waliichakaza goli tatu bila majibu huku kazi kubwa akiifanya golikipa huyu ajulikanaye kama Longino.
Matokeo ya pili, yalikuwa ni ya kitabibu. Longino alikuwa mstari wa mbele kumshauri mfadhili wa timu ile juu ya kila mchezaji kwenda kupimwa afya yake kabla ya ligi ya Wilaya kuanza. Ni ushauri ambao ulikuwa wa maana zaidi kwani walikuwa wamebakiza miezi miwili kuanza ligi hiyo ya Wilaya. Hivyo kabla hawajaianza, ni vyema wangeenda kupima afya zao kuona kama kuna yeyote ana magonjwa yatakayomfanya ashindwe kucheza mpira, likiwemo gonjwa la UKIMWI.
Uzuri matokeo yakaja vizuri kwa wachezaji wote hasa upande wa gonjwa la UKIMWI. Malaria na Taifodi, yalikuwepo magonjwa haya kwa baadhi ya wachezaji, lakini kwa Longino yalipita pembeni. Sasa Longino anarudi nyumbani huku ana majibu mazuri ya kitabibu. Na mdogo wake Jesca alipomuona tu, alishangilia kwa nguvu kama kamuona mwokozi wake wa maisha haya. Jesca alifurahi hadi jino la mwisho likaonekana.
“Umekuja kaka Long.” Jesca aliongea huku akimuaachia kaka yake baada ya kukumbatiana naye.
“Mimi tena dada yangu, lazima nije kuwaona.”Naye Longino alijibu kwa furaha huku akitua mzigo wake mdogo ambao ulikuwa ni begi la nguo.
“Umeniletea nini?” Swali aliulizwa Longino. Longino alipekuwa begi lake dogo na baadae alitoa sweta moja zito na kumkabidhi mdogo wake kipenzi wote wakiwa na furaha kubwa mioyoni mwao. “Asante kaka,”Jesca alishukuru huku akijisogeza na kumkumbatia kaka yake kwa nguvu. Wakati huo mama yake alikuwa bado hajarudi kutoka nyumbani na ni dakika chache tu, Mercy alikuwa ametoka mara moja na kwenda kuangalia mazingira ya kwao.
Longino baada ya kumpa mdogo wake sweta lile, alinyanyua mzigo wake na kutoka pale sebuleni alipokuwepo mdogo wake, na sasa alikuwa ameshika njia ya kutoka ili aende chumbani kwake. Lakini kabla hajamalizikia kutoka, Jesca alimuita tena na kumuambia jambo. Jambo ambalo likazidi kumpa shauku Longino.
“Kaka, Dada Mercy alikuwa hapa sasa hivi. Kasema atarudi baadae kwani kaenda kuangalia hali ya nyumbani kwao.” Jesca alitoa ujumbe huo na kumfanya kaka yake arudi tena na kuanza kumuuliza maswali kadha wa kadha.
“Kwa hiyo anakujaga hapa?” Longino aliuliza.
“Ndiyo. Kila siku anakuja.”Jesca alijibu huku akicheka hadi meno yake yale makubwa ya mbele yakitokeza kuliko mengine.
“Mama anasemaje.”
“Weee, mama anampenda huyo.”
“Hajawahi kumfukuza?.”
“Weee, amfukuze. Nitalia hadi kesho.”
“Kumbe na wewe unampenda eeh.” Safari hii Longino aliongea huku akiwa kachanua tabasamu na kufinya kwa utani shavu la mdogo wake.
“Mimi tena. Yaani asipokuja sili wala silali. Nitamng’ang’aniza mama hadi akamuite.”
“Mmmmh! Dada, huo ukorofi sasa. Unamsumbua mama ee.” Longino aliongea kwa utani huku moyo wake ukiwa na furaha baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa mdogo wake.
“Eee namsumbua. Sasa mimi nitakaaje bila dada yangu.” Jesca aliongea kwa furaha na kumfanya Longino azidi kutabasamu kwa kile kitendo. “Halafu kapika chakula hicho hapo. Njoo hapa tule wote.” Jesca alimuonesha kaka yake chakula kilichohifadhiwa sehemu salama na safi. Sehemu ambayo itakifanya kisipoe haraka na kupoteza ladha yake.
“Haya kadadaa, ngoja nikabadilishe nguo halafu nitakuja kukulisha. Si wajua ni muda mrefu sijakulisha.” Longino alimwambia mdogo wake.
“Aka, Sasa hivi nakula mwenyewe, sitaki kulishwa na mtu.”Jesca alipinga vikali na kumfanya kaka yake awe anacheka huku anatoka mule sebuleni. **** Baada ya kupata chakula kile alichoandaliwa na Mercy. Longino alienda chumbani kwake ambapo alipitiwa na usingizi mkali kutokana na uchovu wa safari na michezo waliyoicheza ambayo iliendana pia na mazoezi magumu.
Mida fulani ya jioni, Longino alihisi kitu kizito mgongoni kwake. Alijitahidi kuinuka lakini alishindwa. Ndipo alipojikakamua kutoka usingizini na kuangalia ni nini kipo mgongoni kwake. Hapo ndipo alikutana na sura mwanana ya kimwana Mercy ikiwa imechanua tabasamu la haja huku amemkalia mgongoni.
Longino alijitahidi kugeuka na kumweka Mercy akae ile sehemu ilipozipu ya suruali yake. Aliofanikiwa hilo alimuangalia mwanadada yule, jinsi alivyokuwa mzuri. Kisha akakumbuka maneno aliyoyaongea mdogo wake. Kichwani Longino alijisemea kuwa Mercy ndio anafaa.
“Mambo totoo.”Mercy alianza kumsalimia Longino huku bado haishiwi tabasamu.
“Poa. Niambie totoo wangu.”Longino naye alijibu huku akijaribu kunyoosha mkono wake na kushika nywele nzuri za Mercy. “Mimi nimeku-miss hapa.”Mercy aliongea kwa deko huku akilala kifuani kwa Longino na kujiachia kana kwamba ameshaolewa na mwanaume yule.
“Totoo, utanishinda mimi kweli? Hapa nahisi kama nipo ndotoni kukuona.”Longino alimjibu huku akiupapasa mgongo wa Mercy ambao ulikuwa umebinuka kwa juu kutokana na ule ulalaji wake.
“Muongo wewe, mbona hukunipigia simu na kusema umerudi, hadi nimekuja hapa ndio dada akaniambia umekuja.” Mercy alizidi kuongea kwa deko huku mashavu kayavimbisha na kufanya sauti yake kutoka kama mtu aliyejaza mate mdomoni.
“Hamna Totoo, nilitaka nikupigie baada ya kupumzika, sema sasa umeniwahi.”Longino alijitetea.
“Wewe hunipendi Long.” Mercy aliongea huku akizidi kujikita kifuani kwa Longino.
“Hamna bwana Totoo, nakupenda sana mamie.” Longino alibembeleza.
“Sitaaakiiii.”Mercy alikuwa kama mtoto anayekataa pipi iliyolambwa na wakati ipo hiyohiyo moja.
0 Comments